PAMBANO LA CHUPAK CHIPIND LAOTA MBAWA.

                                    Raisi wa TPBO, Yasin Abdallah (Ustadhi)

Pambano la ngumi za kulipwa kati ya bondia Laslio Hubert wa Hungury na Chupak Chipindi toka mjini Makambako, limehairishwa kutokana muandaaji wa pambano hiloZoltani Petray kupatwa na matatizo.

kwa mujibu wa taarifa toka kwa  raisi wa ngumi za kulipwa nchini Yasin Abdallah amesema Zoltan amepatwa na tatizo la kuuguza mwanae alievunjika mguu baada ya kuvamiwa na majambazi huko nchini Huangury.

kwa upande wake wakala wa ngumi Franklyn Imbezi kutoka nchini Kenya amesema pambano hilo litachezwa baada ya wiki mbili hadi tatu kulinga na ratiba itakayo tolewa na muandaaji.

0 comments:

Post a Comment