Shirikisho la Ngumi la Kimataifa
Africa (IBF/Africa) limemteua ndugu Miraji Mrisho Kikwete kuwa Makamu wa Rais
anayeshughulikia maendeleo ya vijana katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati hukua akisisitiza kuwa uteuzi huo unaanza utekelezaji wake
mapema mwezi huu.
Rais wa IBF katika bara la
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Onesmo Ngowi amesema kuwa Miraji
ana uwezo wa kuwahamasisha na kuwaunganisha vijana katika shughuli za maendeleo
ya mchezo wa ngumi kimataifa.
Aliongeza
kuwa kuteuliwa kwa miraji ni fahari kwa watanzania na kutaongeza mchango mkubwa
wa kukuza vipaji kwa mabondia vijana waliopo nchini.
Ni muda
mrefi sasa michezo wa ngumi za ridhaa na kulipwa imekosa muamko mzuri katika
mataifa ya Afrika kutokana na kutokuwepo kwa wainuaji wazuri wa michezo hiyo.
0 comments:
Post a Comment