MANCINI AMPA NAFASI 100 BALLOTELI



 Roberto Mancini and Mario Balotelli are separated
                                Ilivyokua ausbuhi ya jana.
Siku moja baada ya kocha wa Manchester City, Roberto Mancini, kuripotiwa kukwaruzana na mshambuliaji wake Mario Balloteli, hii leo meneja huo ametoa utetezi kwa mchezaji wake.

Akitoa ufafanuzi juu ya tukio Mancini amesisitiza kutoa nafasi mia moja kwa nyota huyo huku akifuta hukumu iliyotazamiwa kutolewa kwa Balloteli.

Mancini amesema Balloteli ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 22 anaweza kukosea lakini pia bado ana muda wa kubadilika kutokana na matendo yake.

Katika taarifa yake hiyo Mancini amekana kuwa hakuwa na ugomvi kati yake ya Balloteli mbali na tafsiri ya picha zilizosambazwa na wanahabari juu ya tukio hilo.

Asubuhi ya jana Balloteli alishikana kocha wake baada ya kukemewa juu ya rafu alieyocheza kwa mchezaji mwenzake Scot Sinclare.
MWISHO.

0 comments:

Post a Comment