KIKOSI kamili cha Simba kinaondoka jijini Dar es Salaam kesho
kikiwa na msafara wa watu 18, wakiwamo wachezaji 18 na viongozi saba.
Wachezaji
wanaoondoka ni Juma Kaseja, Abel Dhaira, Nassor Said Masoud, Amir
Maftah, Koman Bili Keita, Juma Nyoso, Shomari Kapombe, Salim Kinje,
Ramadhani Chomboh, Amri Kiemba, Haruna Moshi, Kiggi Makasi, Abdallah
Seseme, Amri Kiemba, Haruni Chanongo, Mrisho Ngassa, Felix Sunzu na
Abdallah Juma.
Viongozi ni Zacharia Hans Poppe,
Muhsin Balhabou, Patrick Liewig, Jamhuri Kihwelo, Dk. Cosmas Kapinga,
James Kisaka na Kessy Rajab.
Simba inaondoka kwa
ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways) majira ya saa 11:10
alfajiri na inatarajiwa kufika Luanda, Angola majira ya saa nne
asubuhi.
Timu itafanya mazoezi ya mwisho jijini
Dar es Salaam leo jioni kabla ya kuelekea kambini ambapo wachezaji
watapumzika kusubiri muda wa safari.
Mechi kati ya
Simba na Libolo itachezwa Machi 3 (Jumapili ijayo) katika Uwanja wa
Calulo uliopo katika mji wa Calulo jimbo la Kwanza Sul (Kwanza Kusini).
0 comments:
Post a Comment