Kocha
wa klabu ya Los Angeles Laker Mike Brown ametimuliwa kazi ya kuinoa timu hiyo
ya kikapu baada ya kuanza vibaya msimu wa ligi ya NBA kule nchini Marekani.
Mike
Brown alishindwa kuanza vema katika michuano hiyo baada ya kufungwa mechi nne
za awali za ligi hiyo kubwa ya kikapu ulimwengu.
Baada ya kufukuzwa Brown amewashukuru viongozi
na wachezaji wa Lakers kwa ushirikiano alioupata kwa muda wote wa kazi
aliyoifanya ndani ya Lakers.
Baada
kufukuzwa kwa Brown kocha msaidizi wa timu hiyo Bernie Bickerstaff alikiongoza
kikosi cha Lakers kwenye mchezo wa leo dhidi Warriors na kushinda kwa
vikapu 111 kwa 77.
0 comments:
Post a Comment